Uvutaji wa sigara umekuwa ukipingwa sehemu mbalimbali duniani hata kupelekea kutungwa sheria mbalimbali ambazo zitaweza kufanya uvutaji wa sigara ukapungua, kuna nchi ambazo uvutaji wa sigara hadharani umekatazwa ukikutwa unavuta ni kosa ambalo linaweza kukupeleka jela au ukalipa faini au vyote kwa pamoja kwa kukiuka sheria hiyo.
Kwa upande mwingine makampuni ya kutengeza sigara sehemu mbalimbali hapa duniani ndiyo yamekuwa yakiongoza kwa kiasi kikubwa kwa ulipaji wa kodi, kutoa ajira za uhakika na kutoa misaada katika jamii za nchi husika.
Katika nchi nyingi katika kupiga vita uvutaji wa sigara, matangazo ya sigara katika televisheni, redio na mabango makubwa ya barabarani yalipigwa vita. Sheria nyingine ikatungwa kwamba kwenye kila pakiti ya sigara maandishi ya kuonya uvutaji wa sigara yakawekwa.
Katika kuendelea kupiga vita uvutaji sigara mfano nchini Australi pakiti ya sigara kwa 65% imetakiwa kuzungukwa na maonyo ya uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya na kuweka picha ambazo zinaonyesha jinsi uvutaji wa sigara ulivyowaathiri, kufanya ile pakiti mtu asione fahari kuwa nayo na kuweza hata kuweka mezani na kuhisj ni fahari.
65% Ya Pakiti Ya Sigara Yatakiwa Kuwa Ni Maonyo
Next Story
Zimbabwe Yakubali Kutumia Pesa Ya China Yuan
Related Posts
-
-
Video: Obama’s Complete Nelson Mandela Memorial Speech
-
Khole Kardashian Awa Kwanza Kufika Hospitali Baada Kim Kardashian Kujifungua
-
Floyd Mayweather Ashtakiwa Na Mpenzi Wake Wa Zamani
-
Documentary ya Beyonce “Life is but a dream”
-
Askari wa Afrika Kusini wamfanyia unyama Kijana wa kisumbiji
-
Desmond Tutu Aunga Mkono Sheria Ya Kujitoa Uhai, Akikiita Ni Kitendo Cha Heshima