- Aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Israel, Ariel Sharon, Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuugua ugonjwa wa kupooza toka mwaka 2006 wakati akiwa kwenye zama za juu za maisha yake ya kisiasa.
Hali yake ilizidi kuzorota katika siku za karibuni na kufanya baadhi ya viungo vyake kushindwa kufanya kazi ikiwemo figo zake.
Bwana Sharon ni mtu muhimu kwenye historia ya taifa la Israel tangu akiwa jenerali wa jeshi na baadaye mwanasiasa.