
Aliyetakiwa kuuawa kutokana na kuzaliwa akiwa na ulemavu wa viungo na kichwa chake kikiwa juu chini awa mwamasishaji mkubwa Brazil.
Claudio Viera de Oliveira mwenye umri wa miaka 37 anayetokea katika mji wa Monte Santo nchini Brazil alizaliwa akiwa na ugonjwa wa arthrogryposis ambao unaathiri viungo vya mwili.
Madaktari walimshauri mama mzazi wa Claudio asitishe kumnyonyesha mwanaye huyo mlemavu ili afe kutokana na njaa, wakiamini kuwa mtoto huyo atakuwa mzigo kwa wazazi wake na wote wanaomzunguka.
Claudio aliwashamgaza watu wote pamoja na madaktari hao baada ya kufanikiwa kupata shahada ya kwanza ya Uhasibu na amekuwa mzungumzaji mwamasishaji (public and motivational speaker) katika midahalo mingi ya kijamii nchini Brazil.
Arthrogryposis ni ugonjwa unaosababusha viungo kushindwa kufanya kazi hasa miguu ya mwathirika wa ugonjwa huo.
