
Msimu mwingine wa ligi kuu ya Uingereza unaanza tena leo Jumapili 2 Agosti 2015 wakati mabingwa wa ligi hiyo Chelsea atakapokutana na bingwa wa kikombe cha FA Arsenal The Gunners katika kombe la ngao ya jamii katika uwanja wa Wembley. Mechi hii inakuja baada ya siku 64 baada ya Arsenal kumaliza mechi za ndani kwa kushinda 4-0 dhidi ya Aston Villa.
Pande zote zimebadilika kwenye vikosi vyao katika msimu wa kiangazi, ingawa kipa Peter Cech atakuwa akicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya timu yake ya zamani ya Chelsea.
Mchezaji mpya wa Chelsea aliyechukuliwa kwa mkopo kutoka Man U anaweza kuanza leo.
Falcao mwenye miaka 29 alitumia msimu wake uliopita akiwa na Man U lakini aliendeleza rekodi mbaya akifunga magoli manne tu kwenye mechi 29.
Alisaini deal la muda mrefu kwa mkopo akitokea Monaco mapema msimu wa kiangazi, Chelsea imesaini golikipa mmoja tu kutoka Stoke ambae ni Asmir Begovic.
Cech mwenye miaka 33, akiwa Chelsea amecheza misimu 11 akiwa Stamford Bridge kabla kusaini dola ya pauni milioni 10 kuhama kutoka Chelsea kwenda Arsenal.
Meneja wa Chelsea Jose Mourihno amethibitisha kwamba mshambuliaji Diego Costa na Mlinzi Gary Cahil wako fit baada ya kupata majerahavmwanzoni msimu.
