B Ball Kitaa tournament kwa mara nyingine imerejea kwa kasi, B Ball Kitaa chini ya mataa ikiwa chini ya udhamini wa Sprite ilizinduliwa siku ya Ijumaa 24 Julai 2015 katika viwanja vilivyopo barabara ya Ocean road jijini Dar es salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mratibu wa B Ball Kitaa Chini ya mataa Reuben Ndege a.k.a Nchakali alisema msimu huu B Ball Kitaa chini ya mataa imekuwa zaidi kwasababu inahusisha timu za mpira wa kikapu kutoka mikoani mfano Arusha, Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Dar es salaam ikiwa na timu zaidi ya 3.
Zawadi kwa msimu ni shilingi milioni 5 kwa bingwa, ambapo kocha wa timu atachukua milioni 1 na wachezaji milioni 4, akizungumza katika uzinduzi Karabani ameombacmashabiki kujitokeza kwa wingi kuanzia siku ya Jumapili 26 Julai 2-15 kusupportvmchezo huo, ikiwa na lengo la kuinua vipaji na kukuzavmchezo wa kikapu zaidi.
Burudani usiku huo ilitolewa na wasaniibwa hip hop akiwemo Izzo B, Weusi, Wakazi, Songa,One Tne Incredible na wengine, chini ya usimamizi wa dj mkali kutoks Magic FM Dj Tass The Talent survivor.