
Wakati Nick Minaj akiwa anashinda tuzo,upande wa pili mdogo wake Nick Minaj anatokutana na vitu tofauti, kutokana na ripoti kutoka Associated Press mdogo wake Nick Minaj anayeitwa Jelani Maraj alikamatwa kwa kosa la ubakaji.
Maraj alikamatwa kwa hilo akituhumiwa kumbaka binti wa miaka 13 mara 3 kati ya mwezi Aprili na Novemba,.
Kaka yake Nick Minaj mwenye umri wa miaka 37, alikamatwa siku ya Jumanne lakini muda mfupi alihamishiwa Nassua University Medical Centre kutokana hali ya matibabu yasiyojulikana, muda mfupi Maraj aliachiwa baada ya kulipwa dola 100,000 kama dhamana.
Vyanzi vya stori vimedhibitisha Minaj alilipa dhamana hiyo ya kaka yake lakini Nick Minaj hajasema chochote kuhusu kesi hiyo wala kuongelea dhamana hiyo.
Damu nzito kuliko maji,haishangazi mtu kumsaidia ndugu yake kama anaweza kufanya hivyo.
