
Wiki hii nzima toka ilipofanyika Grammy 2015 matukio mbalimbali yamekuwa yakiripotiwa baada ya kufanyika tuzo hizo, lakini kubwa ni lile la baba North, Kanye West kutishia kwenda kwenye jukwaa baada ya mshikaji Beck kutangazwa kuwa yeye ndiye mshindi wa tuzo ya “Album bora ya mwaka”. Kanye alizidi kusababisha maneno kuwa mengi baada ya kuongea kwenye mahojiano na kituo cha E!! .
Watu wengi walidhani anatania akiigiza kitendo kile cha VMA pale alipopanda kwenye jukwaa na kusema kwamba Swift hakustahili tuzo aliyokuwa ameshinda bali alistahili kushinda Beyonce.
Alipoongea na E!! alisema “Ni kama najua tu kwamba Grammy, kama wanataka wasanii wa ukweli kuendelea kurudi, wanatakiwa waache kutuchezea, Hatuchezi nao tena na Beck anahitajika kuheshimu usanii na alitakiwa arudishe tuzo yake kwa Beyonce” alifunguka Kanye West.
Akiongelea tukio hilo wakati akipiga stories na Us Weekly, Mkali huyo Beck ambae aliachia ngoma inayoitwa “Loser” mwaka 1994 wala hakuchukizwa na alichokifanya Ye. Wengi walidhani West anajoke lakini alipohojiwa alisema kweli Beck hakustahili.
Beck Aliendelea kumuita Kanye West “genius” na aliendelea kusema kwamba alidhani kwamba Beyonce ndiye ambae angeshinda tuzo ile usiku ule pale” Alifunguka Beck.
Nilishangazwa alikuwa anakuja kwenye jukwaa, anastahili kuwa kwenye jukwaa kama mtu mwingine yeyote, Ngoma ngapi ametoa kali katika miaka mitano iliyopita? alisema Beck
Waandishi wa habari walipokutana na Kanye West katika uwanja wa ndege huko katika jiji la New York, alipoulizwa alisema Beck hakuwa msanii aliyestahili, aliongelea sana sana kuhusu Grammy na sio Beck.
Na hii sio mara ya kwanza kwa Kanye West kufanya kitendo kama hiki alishawahi kupanda kwenye jukwaa na kusema Taylor Swift hakustahili tuzo aliyopewa.
