Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema hadhani ni sawa kurejesha fedha za umma zilizotumiwa kukarabati nyumba yake binafsi kwa sababu hakuwahi kutoa pendekezo hilo….
Bw. Zuma amesema haoni haja ya kuchangia pesa zake binafsi katia ukarabati wa nyumba hiyo kwani halikuwa pendekezo lake toka mwanzoni.
Kadhalika bwana Zuma ameiambia runinga moja nchini Afrika Kusini kwamba maafisa wa serikali ndio waliopanga ukarabati huo uliogharimu dola milioni 23 bila kumuarifu…Hii ndio mara ya kwanza Rais Zuma amezungumzia kuhusu makaazi hayo yaliyozua mjadala mkali wa umma Afrika Kusini.