Kipindi Cha nyuma Kutokana Na majanga mengi yaliokuwa yanamkuta Justine Bieber kutokana na kupenda sana kwenda club na kujikuta matatani akiwa njiani kurudi nyumbani kwa kuendesha gari akiwa amelewa au vyovyote, Miley Cyrus alimshauri Bieber anunue nyumba yenye Night Club ndani ili kumuepusha na yote hayo
“Una pesa nyingi sana, nunua nyumba yenye night Club” alisema Miley
Hatimae Justine ameonekana kufuata huo ushauri baada ya kuhama nyumba aliyokuwa amepanga huko Beverly Hills condo na kuhamia Hollywood hills kwenye bonge ya mjengo wenye nigt Club ndani so kwa sasa kijana huyo atakuwa na uwezo ku party atakavyo humo ndani na marafiki zake bila kupatwa na majanga yeyoye..
Ukubwa wa 16,000 square Ikiwa ni ya vioo vitupu , ndani yake kukiwa na bar tatu, taa na mziki mnene , pia humo ndani kuna gym iliyojitosheleza kila kitu , pool table,ping pong enclave, vyumba kumi vya kulala huku kukiwa na master suites zenye kila aina ya nguo lakini zaidi pia jumba hilo linapatikana ukumbi wa sinema ndani yake wenye tv yenye ukubwa wa 160-inch