Mfanyabiashara mmoja aliyefahamika kwa jina la Malam Yahai, ameburuzwa mbele ya mahakama huko Garki LGA Jigawa State nchini Ethiopia baada ya kutuhumiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 14 na kumpa mimba. Binti huyo (14) ameshurutisha mtuhumiwa huyo achukue jukumu la kumtafutia mtoto huyo anayetegemea kuzaliwa jina , ikiwa nakupeleka nguo kwa mtoto huyo wa kiume limeripoti Vanguard. Akielezea tukio hilo mbele ya mahakama binti huyo ambae anafanya kazi kama mfanyakazi wa ndani kwa mke wa Malam Yahai, anasema Yahai ameshambaka zaidi ya mara moja. Alisema Yahai kila wakati aliganya hivyo mke wake alipokuwa hayupo “Mheshimiwa siwezi kueleza ni mara ngapi alinibaka” Mtuhumiwa pia alishtakiwa kwa kosa la kutoa rushwa ya N300,000 ili polisi wamalize kesi hiyo. Na hayo yote, mtuhumiwa Malam Yahai alikutwa hana makosa
kutokana na mashtaka hayo.