Mshiriki wa Tanzania Nando Amefukuzwa kutoka nyumba ya Big Brother baada ya kushindwa kutimiza vigezo na Mashart ya Nyumba hiyo Baada ya kuanzisha ugomvi Na mshiriki kutoka Ghana Eliken siku ya Ijumaa.
Nando ndio alikuwa kinara wa ugomvi huku maneno makali na mazito yakimtoka kumtusi Elikem huku kaka hyo wa ghana akionekana kucheka na kumtaka Nando amatafute baada ya mashindani na sia hapo ndani.
Kiburi na ajeuri ya Shombe shombe huyo wa kibongo ambaye alikuwa anadhihirisha utoto wake aliendelea kumtusi matusi makubwa bwana Elikem huku akimtishia kumuua kwa kuwa yeye nando aliamini sio reak Nigga kama alivyosema mwenyewe
Ikiwa haitoshi hata maara baada ya ugomvi ili kuthibitisha kuwa nia yake ya kumuua Elikem ipo akilini mwake alionekana kutembea na kisu wazi wazi tena akikinoa kuashiria anasilaha inamlinda na wakati wowote ni show time, haikuwa mara ya kwanza kwa Nando kutembea na kulala nacho akikihifadhi chini kitanda chake kwani alishaonywa na Kaka Mkubwa mara baada ya kuonekana na kisu usiku wa channel O party.
Hata hivyo biggie nae alishindwa kuvumilia makosa ya Nando ambaya yalionekana kuhatarisha sio tu maisha yake bali hata ya wenzake, hivyo Bigie alitumia wasaa huu wa siku ya mtoano ambapo mara baada ya washiriki AnnaBell Wa Kenya na Sulu wa Zambia kuyaaga mashindano Biggie aliwataka washiriki wote kukusanyika living room kisha akawakumbusha washiriki baadhi ya Masharti na vigezo lakini kusikitishwa na wengine ambao wamekuwa wakiyafanya huku wakijua wanafanya makosa.
BIGGIE ALIMUITA nando Diary Room Na kumkumbusha makosa ya Ugomvi, kutumia maneno makali, na kutaka kupigana huku akitembea na kulala na kisu huku akijua ni Makosa, Hivyo Biggie aliwataarifu washiriki waliosalia pamoja na Nando kuwa Hapo ndio ulikuwa Mwisho wa Mchezo huo kwa Mshiriki Nando.
Bahati mbaya ilizidi Kwa Nando baada ya kutopewa hata nafasi ya kuagana na washiriki wenzie kwani safari yake ya kuondoka ilimalizikia hapo hapo Diary Room bila kupewa nafasi hata ya kukusanya mizigo yake ambapo mshiriki wa Ethiopia Bimp ambaye ndio alikuwa Rafiki mkubwa wa Nando akionekana kumkusanyia mizigo yake.
hasira Hasara , Majuto ni Mjukuu.
Karibu Uraiyani Nando.