Washiriki Feki wakiwa Diary Room baada ya kustukizwa kuwa safari yao mdio imeishia hapo wakiwaaga washiriki halali kupitia Scree iliyopo living room
Kutoka ndani ya nyumba ya Big Brother wiki hii moja kati ya matukio makubwa ni lile la washiriki feki kutlewa ghafla bila yeyote kutegemea kuanzia real house mate mpaka watazamaji na wao wenyewe, washiriki hao waliokua wanajulikana kama Emerald Housemates walijikuta wakiyaaga mashindano hayo mara baada ya kumaliza Task waliokuwa wamepangiwa waifanye ya kuigiza wakishiriki pamoja na washiriki halali,
Badaaya ya mchezo wao huwa wa kuigiza kuisha kama kawaida walitakiwa kuingia sebleni ila kupewa majibu yao ya kama wameshinda au la, lakini kabla ya hayo washiriki hao feki wote waliitwa Diary Room na Big bila yeyote kufahamu waliitiwa nini, baada ya kuingia Big aliwasha Tv iliyopo sebleni ili kuwafanya washiriki halali kuwaona washiriki hao fake kutokea chumba hicho cha Diary.
Ndipo Big akawafungukia washiriki hao kuwa safari yao imeishia hapo huku akiwajuza washiriki halali kwamba hao walikuwa washiriki feki Jambo lililozua mshangao kati yao wote washiriki halali ya kwamba wale hawakua washiriki halali na washiriki halali kuondoka ndani ya jumba hilo bila hata kuagana na washiriki halali.
Nando akimsemeza Elikem masikioni mwake wakati wa ugomvi
katika hatua nyingine siku ya ijumaa usiku kuliibuka ugomvi mkubwa baina ya Nando wa Tanzania na Elikem wa Ghana ugomvi ambao chanzo chake sojakifahamu zaidi ya kukutana na usuluhishi kesho yake uliokuwa unazungumzia kuibiana kufichiana na kunyimana Pombe, hata hivyo Nando alifikia hatua mbaya baada ya kutaka kumvamia Elikem jambo ambalo lingemfanya awe amevunja miiko ya mashindano hayo na angetolewa lakini kwa bahati wa waamuzi wa ugomvi huo Bimp wa Ethiopia na Melvin wa Nigeria kuwa tenganisha na iliobaki ikawa ni mashambulizi ya maneno ambapo Nando ndio alionekana kuongea zaidi na kutoa matusi makali sana kwa Elikem huku Elikem akionekana kucheka na kumrudishia majibu ya kwamba kama anataka amtafute akiwa nje ya mjengo ndo atamuelewa Other wise kwa pale ndani atakua anacheza tu kiduku