Bunge maalumu la katiba limeunda kamati 12 za kujadili na kupitia rasimu ya katiba kifungu kwa kifungu na kisha kuwasilisha maboresho na mapendekezo katika rasimu hiyo bungeni kwa ajili ya kutengeneza katiba inayopendekezwa na kisha katiba hiyo kupigiwa kura ya maoni na wananchi ili kupata katiba mpya.
Akitangaza kamati hizo 12 mwenyekiti wa bunge maalum la katiba Samwel Sita amesema kuwa kila kamati atapewa baadhi ya vifungu katika rasimu ya katiba hiyo kwa ajili ya kupitia na kufanya maboresho ikiwa ni pamoja na kutoa mapendekezo na kisha wenyeviti wa kamati hizo watawasilisha mapitio hayo bungeni ili kujadiliwa na bunge hilo kwa ujumla .
Mara baada ya mwenyekiti kutangaza kamati hizo na kutoa fursa kwa wajumbe kugombea nafasi za uwenyekiti wa kamati kukaibuka hoja kwa baadhi ya wajumbe wakidai uwingi wa wajumbe kutoka chama tawala huenda ukasababisha kamati hizo kutawaliwa na wanachama wake huko nao baadhi ya wajumbe kutoka visiwani wakihoji wingi wa wajumbe kutoka bara huenda ukawanyima fursa ya kupata nafasi hiyo.