Chriss Brown anasema jela ilikuwa fresh sana na kwamba jinsi alivyokuwa akihudumiwa ilikuwa ni vizuri zaidi.
Chriss ambaye aliongezeka sana alipokuwa jela anasema uzito aliokuwa nao ulimbadilisha kwa kiasi kikubwa.
“Uzito wangu wa kawaida ni kama kilo 180, nilipotoka jela nilikuwa na kilo 215, niliwaza sana inakuwaje kwa sababu hata jeans yangu ilikuwa hainitoshi, hata nguo yangu yeyote, niliogopa kutoka nje, niliona kama watu sijui watanionaje, naonekana mnene, baada ya muda mfupi, nikaenda kucheza basketball muda mwingi, mazoezi mengi, alafu nikafanya video ya wimbo wa “New Flame” tulifanyia mazoezi sana na tunzo za BET na show nyingine, kila wakati nilikuwa nikicheza, najaribu kurudisha mwili wangu kwenye shepu yake” alisema Chriss Brown wakati akipiga stories na Extra Mario Lopez.
Nje ya mabadiliko ya uzito wake, anasema pia kuwa jela ilimfundisha zaidi kujitazama, ni kitu ambacho hawezi kusahau, kwa sasa Chriss Brown anasema hafanyi vitu vya kipumbavu akiwa kama mtu wa kawaida na Chriss Brown kama msanii kitu anachotaka kuonyesha.
Na kwake kila wakati ndivyoilivyokuwa ila sasa hivi ni zaidi na ipo hivyo na pia anafanya hivyo. Chriss Brown anasema amekuwa sasa amekuwa wa tofauti.