Ukurasa rasmi wa CIA umetweet jana Jumatatu 7 kuhusu alipo Tupac na kusema Hawajui Tupac alipo. Tupac aliuliwa kwa kupigwa risasi mwaka 1996 na kesi yake mpaka leo bado haijulikani ni nani alihusika na mauaji hayo.
Mwezi Mei mmiliki wa Death Row Records Suge Knight sehemu ambayo Tupac alirekodi alisema repa huyo yuko hai.
Kwa nini unadhani hakuna mtu aliyekamatwa kama walisema wao ndio kati ya waliomua, kwa sababu Tupac hajafa, Tupac hajafa, kama angekuwa amekufa wangekuwa wamewakamata wale waliohusika, unajua yuko sehemu anasmoke Cuban cigar kwenye kisiwa Fulani alisema Suge Knight.
Tweet Ya CIA ilisemea Hatujui halipo Tupac.