Baada ya kuwepo kwa tetesi za muda mrefu kuhusiana na mpenzi wake na Diamond Platnumz, Penny Mungilwa kuwa mjamzito, hatimaye leo Diamond amethibitisha ni kweli wanategemea mtoto wao wa kwanza.
Nakumbuka tetesi hizi ziliibuliwa na mtandao wa Bongo 5 baada ya kuhisi picha ya Penny akiwa Aiport na kivazi alichokua amekivaa Kama ni mtarajiwa Mzazi au la na baadhi ya watu ku Coment.
sasa leo kupitia Segment ya Radio moja maarufu ya jijini Dar Diamond amefunguka kuwa tayari amempa gari ya kutembelea mrembo huyo huku pia akimuagizia gari mpya aina ya Hyundai ix35.
Nukuu “That’s true, ni kweli unajua sitaki kusema ni mpenzi wangu, sasa hivi ni mama watoto wangu kwasababu ya mizunguko ya kwenda clinic na nini nikaona sio vizuri kwenda kwenye madaladala kugombania… nikaona ni vizuri nikimnunulia gari yake kuendea clinic na vitu vingine. Nimemuaigizia ile new model ya Hyundai ix35.”
Bei ya Hyundai ix35 inaweza kufikia shilingi milioni 50 na zaidi.
Salmamsangi.Com inawatakia kila la Kheri wapenzi hawa katika maamuzi haya mazuri waliofikia.
story credit: Bongo 5