
Mtu yeyote huwa mazingira yanakushape, vitu vilivyokuzunguka unavyoishi navyo na wewe huweza kuchukua tabia za mazingira hayo ukaona fresh hakuna hatari wala usijali kwa sababu ndo maisha yako ya kila siku.
DMX akiwa uwanja wa ndege alipiga stories na TMZ akaulizwa vipi ameshawahi kula chakula cha mbwa akajibu ndiyo.
Wakati wa mahojiano hayo DMX alieleza vyakula vizuri kwa ajili ya mbwa.
“Kiukweli vyakula vya mbwa vinanukia vizuri, lakini bora vina vitamin, madini na virutubisho, Ni vizuri vitamu, ni vyakula vinavyojulikana” Alisema DMX.
DMX kufananishwa na mbwa ameshatokea kwenye makala mengi katika maisha yake ya muziki, huwa anabweka katika nyimbo zake, kuna nyimbo zake zina jina la mbwa “It’s dark and hell yuko na mbwa, Get me dog pia kuna wimbo unaitwa for my dogs, Flesh of my flesh Blood of my blood features dogs for life. 2003 Grand Champ yuko na mbwa kwenye cover.
Albamu hiyo ina dog intro and dog out ikiwa ni moja ya list za ngoma za albamu. Albamu ya DMX;s 2006 iliitwa Year of the dog tena alikuwa na mbwa kwenye cover la albamu hiyo.
Maisha yake amekuwa akiishi na mbwa na mbwa sana akaona hata kula chakula chao ni fresh tu kwa sababu ni kama washkaji zake anawadoea anaona kama wanafaidi.
