
Mkali katika NBA LeBron James kila wakati amekuwa akionyesha mapenzi yake kwenye Hip Hop.
Repa ambae yuko juu ambae yuko namba 4 akiwa na dola milioni 33 katika Cash Kings list 2014 iliyotolewa juzi na Forbes mkali wa ngoma “Started from the bottom” mkali anayewakilisha Canada katika hip hop game Drake amesema yuko tayari kufanya kazi na mkali huyo wa basketball nchini Marekani LeBron James.
Wakati Drake alipokuwa akiondoka katika kipindi cha kwanza cha LeBron cha TV kinachoitwa Survivor’s Remorse, Drake aliulizwa kuhusu kufanya kazi za kimuziki na mchezaji wa Cleveland Cavaliers mkali LeBron.
“Wakati wowote mwanangu, mwambie anicheck” alisema Drake.
Kipindi hicho cha Survivor’s Remorse kitaonyeshwa, ikiwa ni sehemu ya sita, kipindi cha komedi cha dakika 30 kikiwa kimejikita katika kuonyesha maisha na safari ya wachezaji wachanga wa mpira wa kikapu kuwa mastaa, kipindi hicho kinaanza Oktoba 4, 2014.
Cleveland Cavaliers ni timu ya kulipwa ya mpira wa kikapu kutoka mjini Cleveland, Ohio nchini Marekani.
