Dubai imejinyakulia sifa ya kipekee katika kupima Imani za jamii kwa pochi iliyoangushwa mtaani,na ikarejeshwa kwa mhusika mara moja. Katika utafiti uliofanywa na mtengeneza Filamu mwenye asili ya Uingereza katika mitaa ya Dubai, alijaribu mara arobaini na tano kuidondosha kwa makusudi na katika kila tukio msamaria aliyeiokota aliirejesha pochi hiyo kwa mmiliki wake. Daniel Jarvis, mwenye miaka 26,akiwa ameificha kamera yake na kurekodi mfululizo wa matukio hayo ya makusudi akiwa pamoja na rafikiye aliyejipachika jina la utani la ‘Digi’ ama Dan, mwenye miaka 25, walibarizi katika viunga vya Downtown na Bur vilivyoko Dubai,siku za karibuni na kuweka swali je unaweza kuiba Dubai? Kutaka kuichunguza jamii na kurushwa vipande vyake katika YouTube ambapo mpaka kufikia jana usiku watazamaji walikuwa ni zaidi ya 70,000 . Jarvis aliiambia 7DAYS walishangazwa na utafiti huo na kikubwa kilichowasangaza ni kwamba waliookota pochi hiyo hawakujishughulisha kutazama ndani kuna nini? Wakati pochi hiyo ilikuwa imesheni euro za kutosha na fedha ya Falme za Kiarab dirham kadhaa. Mtaa wa kwanza walioufanyia majaribio ni mtaa uliko katika barabra ya Sheikh Zayed karibu na soko kuu la kibiashara na jirani kabisa na mnara wa Emirates lakini kila aliyeiona pochi hiyo aliirejesha,lakini baadaye tukafikiri sababu ya kurejeshwa pochi hiyo kuwa walioko eneo hilo ni matajiri. Basi utafiti wetu tukauhamishia eneo la Bur ,Dubai, mahali ambapo palionekana duni kidogo cha ajabu watu waliendeleza utamaduni ule ule wa kurejesha pochi kama ilivyo, na hali eliendelea hivyo mara kadhaa. Jarvis
anasema wameshafanya utafiti kama huo katika mji wa London nchini Uingereza. Na huko walistaajabu walipoidondosha tu aliyeiokota alianza kukimbia nayo wa nako hakuna aliyethubutu kuichukua pochi hiyo. Jarvis, alivalia suti nadhifu na kuigiza kudondosha pochi anaonekana kwenye video hiyo anaeleza hisia za kurejeshewa kitu ulichondondosha kuwa ni raha iliyoje .lakini akaendelea kusema kuwa anadhani vyombo vya habari hupotosha ukweli,kwakuwa kulikuwa na kichwa cha habari kuwa kuna mtu alihukumiwa miaka 15 jela kwa kuiba mdoli wenye taswira ya dubu, utafiti wetu umegundua tofauti na wayasemayo. Trollstation ina wanachama wapatao 230,000 na utafiti wao kutoka Falme za Kiarab unaelekezwa Ulaya, Marekani na hatimaye Afrika .Inawezekana katika maeneo watakayopita kuvunja rekodi ya Dubai tusubiri wakati uwadie, ni kauli yake Jarvis .