
Leo Waafrika Wamedhihirisha kutokuwa makini kabisa hata kwenye mambo muhimu kabisa baada ya mwanamume anayetajwa kwa lugha ya Thamsanqa Dyantyi mtafsiri wa lugha za ishara kutoka nchini Afrika Ya kusini kutafsiri ndivyo sivyo ishara na maneno yaliokuwa yanazungumzwa na viongozi mbali mbali duniani wakati wa misa ya mzee mandela
Serekali ya Afrika Kusini imesema kampuni iliyomtoa mtafsiri wa lugha za ishara wakati wa ibada ya kumbu kumbu kifo cha Nelson Mandela imekuwa akidanganya kwa miaka mingi na imekuwa ikitoa watafsiri wenye kiwango cha chini.
Wataalamu wa lugha za ishara wamesema mtafsiri huyo wa lugha za ishara, Thamsanqa Dyanty, alikuwa “akitapatapa” wakati wa ibada hiyo siku ya jumanne.
Naibu Waziri wa Afrika Kusini Hendrietta Bogopane – Zulu amesema hakuna suala lolote la kukiuka taratibu za kiusalama wakati mtafsiri huyo alipokuwa akisimama kwani alikuwa na vibali halali.
Katika maoni yake mtafsiri huyo anayelalamikiwa, Bwana Dyanty , amesema alipatwa ugonjwa wa kuchanganyikiwa na hata hivyo alikuwa kwenye matibabu ya akili kutokana na kwamba siku hiyo alijikuta akiskia makelele maskioni mwake hivyo kumfanya kuchanganyikiwa
Kwa upande wake mmiliki wa kampuni iliyomtoa mtafsiri huyo ametupilia mbali madai ya Naibu waziri Bogopane Zulu.
Awali Naibu Waziri huyo aliwaomba radhi jamii ya viziwi kwa kiwango cha chini cha kutafsiri kilichofanywa na Bwana Dyantyi kutoka kampuni ya SA Interpreters.
“Mtafsiri huyo anazungumza lugha ya Xhosa hivyo kiingereza kilikuwa kigumu sana kwake,” alisema Waziri huyo.
