
Aliyewahi kuwa mshindi wa miss Tanzania mwaka 2004, Faraja Kota Nyalandu jana asubuhi alizindua tovuti yake maalum ambayo itajikita katika kusaidia kutoa mawazo mbadala katika kukabiliana na changamoto za kielimu kwa wanafunzi wa shule ya upili lakini kwa O-level.
Faraja alisema katika tovuti hiyo kutapatikana taarifa za habari za kielimu kwa wanafunzi kwa kuzingatia mfumo wa utaala wa ufundishaji ambao umepitishwa ,kuhakikiwa na kukubaliwa na waziri husiku na kukubaliwa na wizara husika kama sehemu ya kuongeza chanzo ama vyanzo vya elim Tanzania
kwa maneno yake Faraja Nyalandu Anasema: “vijana wa sasa wameamka na wameanza kukumbatia ama wamezoea matumizi ya teknologia na hivyo itakuwa ni rahisi kwao kujifunza kwa kutumia mtandao huu ambao utatumia nyenzo na walimu wa shule zenye sifa Tanzania”
Aliendelea kwa kusema sababu kuu za kuzindua tovuti hii ni kuziba pengo la upatikanaji wa habari za kielimu ya upili na pia kuongeza maarifa,uwezo,ujuzi, kubadilishana mawazo kwa njia ya kidijitali na kurahisisha mawasiliano kwa ukaribu baina ya wanafunzi na walimu
Sherehe hiyo ya uzinduzi wa tovuti hiyo ya www.shuledirect..co.tz ilifanyika katika Hotel ya kimataifa ya Serena Jijini Dar Es Salaam na kushuhudiwa na mgeni rasmi ambaye alikuwa naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Philip Mulugo
