
Kama kawa msanii ambaye mara kwa mara amekuwa katika headlines kwa sababu ya beef kibao, beef zake bado hajazila akazimiliza mkali anayewakilisha Compton, The Game amekutana na mshikaji ambae hazipandi kabisa huko California katika klabu ya usiku taarifa kutoka MTV zimeripoti, Game na Lil Durk walirushiana maneno.
The Game alikuwa na washkaj zake na Lil Durk alikuwa na washkaji wake na kurushiana maneno huku ikirekodiwa video na alisikika mtu akisema wakutane nje, Mwezi Mei Game alimdiss Lil Durk kwenye Chiraq To L.A, Mwezi Juni Lil Durk aliulizwa anamtamani mwanamke gani ambae angependa kukutana nae akasema mke wa The Game.
