
Kupitia tuzo za waandishi wa habari zilizofanyika ijumaa usiku pale diamond jubelee hall, Mwanahabari Mkongwe Hamza Kassongo alipata Tuzo ya Mwandishi Wa Habari Mkongwe aliepata Mafanikio
Bwana Kassongo akiwa na moja ya Majaji wa Tuzo hizo.
Mzee Hamza Kasongo mwenye umri wa miaka 74, ni mtangazaji mkongwe wa radio na TV, alikuwapo kama mtangazaji wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kwa mara ya kwanza kwa kutajwa Tanzania badala ya Mungu Ibariki Tanganyika siku ya uhuru mwaka Desemba 9, 1961, ambapo aliwasiliana moja kwa moja na Alex Nyirenda wakati akipandisha mwenge mlima Kilimanjaro.Mzee Hamza Kasongo alikuwa miongoni mwa vijana saba waliochaguliwa kupata mafunzo ya utangazaji wa Sauti ya Dar es salaam, kabla ya RTD miaka ya 60. Baada ya Uhuru, akiwa na hayati Salim Seif Mkamba na David Wakati (RiP) January 1962 walipata nafasi ya kwenda kupata mafunzo ya utangazaji jijini London, Uingereza, katika Shirika la Habari la BBC na kutangaza. Mwaka 1965 alirejea na kuwa mkuu wa habari na matukio RTD. Baada ya miaka kupita akajiunga na Africa Media Group na kuwa Mkurugenzi wa Habari wa Channel Ten ambapo hadi leo anaendesha kipindi cha Wasaa wa Hamza Kasongo.
HAMZA KASONGO HOUR ni kipindi ambacho kimekua kikifananishwa na kile kilichokua cha muda mrefu kilichokua kinaruka CNN na Larry King Live.
Salmamaangi.com inatoa pongezi sana kwa mwanahabari huyu Nguli Kwa Tuzo hiyo ya heshina na kutambulika mchango wake
Hamza Kassongo kupitia tuzo hiyo pia amejinyakulia zawadi ya fedha Taslim Shilingi Millioni Kumi.
