
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 264 zilizofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Misuna manispaa ya Singida.
Kuanzia kulia ni Mwenyekiti Mtendaji HMT, Zena Tenga na Meneja mkuu wa shirika la nyumba (NHC) Nehemia Mchechu na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Queen Mlozi.
Mwenyekiti mtendaji wa Hassan Maajar Trust,Zena Tenga akitoa taarifa yake kwenye hafla ya kukabidhi madawati 264 yaliyotolewa na shirika hilo kwa shule za msingi saba za manispaa ya Singida.
Meneja mkuu wa shirika la nyumba (NHC) Taifa, Nehemia Mchechu akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 264 kwa shule saba za manispaa ya Singida.
Madawati hayo yana thamani ya zaidi ya shilingi 22.5 milioni, yametolewa kwa ushirikiano na shirika la HMT na NHC.
Wanafunzi wa shule ya msingi Misuna wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa halfa ya kukabidhi madawati katika shule yao.Bango la moja kati ya shule saba za msingi mkoani Singida zilizogaiwa madawati hayo.
Shirika lisilo la kiserikali la Hassan Maajar Trust (HMT) kwa kushirikiana na shirika la nyumba la taifa (NHC), limetoa msaada wa madawati 264 kwa shule saba za wilaya ya Singida yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 22.5.
Akizungumza kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Misuna mjini Singida, Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la Hassan Maajar Trust Zena Tenga amesema wamefikia uamuzi huo wa kutoa msaada wa madawati ili kupunguza tatizo sugu linalozikabili shule za msingi na hasa zile za vijijini.
Zena amesema kwa hali hiyo, madawati hayo yatawanufaisha wanafunzi 750 wa shule hizo saba za msingi ambao walikuwa wanakaa sakafuni wakati wa kusoma.
Mwenyekiti huyo mtendaji, amesema lengo lao pamoja na mbia wao NHC, msaada huo utasaidia kukuza viwango na utakuwa chachu ya upatikanaji wa matokeo bora ya mitihani mbalimbali.
Katika hatua nyingine, Mweyekiti huyo mtendaji, alitumia fursa hiyo kulishukuru shirika la nyumba la taifa kwa kuwaunga mkono juhudi zao za kampeni ya ‘Dawati kwa kila mtoto”, ili lengo liweze kufikiwa.Kwa mujibu wa mwenyekiti mtendaji wa
HMT Zena, mfuko wa HMT unalenga katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuendeleza michezo na sanaa kwenye shule mbalimbali Tanzania.“Dira ya HMT ni kuboresha ubora wa vyumba vya madarasa ili kuweka mazingira yanayofaa kwa wanafunzi wote na kukuza upeo na vipaji vya kila mwanafunzi, kimasomo na kiafya.Amesema mfuko huo wa HMT, ulianzishwa kwa ajili ya kumbukumbu ya Hassan Shariff Maajar (Hashy) ambaye alifariki kwa ajali Novemba 11 mwaka 2006.
