Hatimae Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela akazikwa katika kijiji cha Qunu mkoa wa Cape Mashariki nchini Afrika Kusini.
Mjane wa Mandela Graca Machel pamoja na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma walikuwepo katika hafla ya mazishi iliyohudhuriwa na jamaa wa karibu wa familia ya Mandela pamoja na viongozi wengine wakuu.
Takriban watu 4,500 ikiwemo wageni wa kimataifa walihudhuria mazishi hayo ambayo yalikuwa ya mchanganyiko wa tamaduni za kale na mambo ya kisasa wakati ambapo familia ya Mandela Ilikesha Usiku Kucha wakijiandaa Kumzika Mtu wao
Ibada Za Kimila Ni Moja ya matukio muhimu yaliofanyika huku kiongozi mmoja wa kimila akiita Mizimu na kuzungumza na mwili wa mandela kuwa sasa anazikwa
Hayati mandela ndio Rais wa kwanza mzalendo wa Africa Kusini Baada ya kutumikia kifungo cha miaka 27 Jela
Mandela alifariki tarehe 5 mwezi Disemba akiwa na umri wa miaka 95.
Mizinga 19 ilipigwa kama ishara ya heshima kwa jemedari huyo kabla ya kumzika, Mandela Alifariki akiwa na umri wa miaka 95 baada ya kuugua mapafu kwa muda mrefu ugojwa aliopupata Jela kutokana na kazi ngumu,
ikumbukwe wakati wa mazishi yake kuiwashwa mishumaa 95 kama ishara ya miaka yake aliyoishi hapa duniani
kitu kingine kizuri ni heshima na stara aliyoistahili Nelson mandela kwa kutoonyeshwa live wakati anaingizwa kaburini lakini pia kutopatikana kwa picha yake akiwa mfu katika jeneza na kuwafanya waliohudhuria tu ndio kushuhudia tukio hilo.
Tazama picha kumi muhimu hapa katika tukio hilo
Jeneza La Tata Madiba likionekana vizuri kupitia kituo cha luninga cha SABC ambacho ndicho kilichokuwa kinarusha matangazo yake Live
Mwili wa Tata Madiba Ukisindikizwa kuingizwa katika kijiji alichokulia Qunu
Mjane Wa Marehemu Nelson Mandela Graca Machel, akifuta machozi wakati wa ibada ya mwisho ili kumzika mume wake mpezi
Mke wa Zamani wa Raid Nelson Mandela Winnie Mandela Madikizela, Na mjane wa marehemu Nelson Mandela, Graca Machel , wakiwa wamesimama mbele ya jeneza la mpendwa wao
Mjukuu wa Rais Mandela Nandi Mandela akizungumza wakati wa ibada ya mazishi ya kumzika babu yake
Kiongozi wa kiroho Desmond Tutu akiwa kakumbatiana na Rais Mstaafu Wa Afrika Kusini Thabo Mbeki wakati wa mazishi ya Nelson Mandela
Rafiki wa karibu sana na Raid Mandela Ahmed Kathrada akizungumza mbele ya umati uliohudhuria mazishi yake
Watoto wakicheza pembeni ya Maturubai yaliojegwa rasmi kwa ajili ya ibada ya mwisho ya kumuaga Tata Madiba Huko Qunu
Kijana katika taswira ya kuuza magazeti huku picha ya mbele ikimuonyesha mke wa zamani wa Mandela na Mjane wa Mandela
Familia Moja ilijikusanya pamoja ilitazama Luninga Kushuhudia Maziko ya Mkombozi wao