Bunge limeingia kwenye tafrani na mvutano mkali, baada ya Naibu Spika wa Bunge Bw. Job Ndugai, kuamuru kutolewa nje kwa kiongozi wa upinzani bungeni Bw. Freeman Mbowe, na wabunge wa upinzani kuzuia kiongozi huyo kutolewa ukumbini.
Hii ndiyo hali ilivyokuwa ndani ya ukumbi wa bunge huko mjini Dodoma, ambapo mbunge wa Mbeya Mjini Bw. Joseph Mbilinyi alianza kutolewa nje, kutokana na kuzuia kiongozi wa upinzani bungeni asitolewe nje ya ukumbi wa bunge. Kuja kwa amri hiyo ya naibu spika, ilikuja mara baada ya Kiongozi wa Upinzani bungeni kukataa kutii mamlaka ya kiti ya kukaa chini ili kupisha mjadala wa muswaada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba wa mwaka 2013, uendelee.
Agizo la kutolewa nje kwa mbowe Mara baada ya Bw. Mbowe kutoka nje ya ukumbi wa bunge, tafrani iliamia nje ya ukumbi huo baina ya wabunge wa upinzani na askari wa bunge waliotokeleza amri ya naibu spika.
Kutokea kwa tafrani hiyo kulitokana na mbunge wa Mkoani, Bw. Ali Khamis Seif kuomba muongozo wa spika, akitaka hoja iliyokuwa mbele ya bunge iharishwe, na Naibu Spika kuamua kuitisha kura za kutounga mkono au la, ambapo wabunge wasiounga mkono wakashinda.
Mchungaji Peter Msigwa Pamoja na tafrani hiyo, Mjadala wa muswaada wa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba uliendelee, na kabla ya kusitisha kikao, Naibu Spika akatoa msamaha kwa Kiongozi wa Upinzani na wabunge walioleta tafrani ndani ya bunge.