Historia imeendelea kuinnyong’onyeza Uholanzi, historia inaonyesha mara nyingi timu ya Uholanzi imekuwa ikifanya vizuri katika mechi zake za fainali za kombe la dunia na kufika mbali lakini haina bahati ya kulinyakuwa kombe hilo.
Mwaka 2010 nchini Afrika kusini Uholanzi alifanikiwa kufika fainali dhidi ya Hispania lakini ilifungwa na kushindwa kutwaa ubingwa.
Jana Uholanzi tena ikiwa katika mechi ya nusu fainali kuelekea fainali ikiwa na rekodi nzuri kabisa katika kombe la mwaka huu ilishindwa kutamba mbele ya Argentina baada ya kufungwa kwa penati 4 kwa 2.
Pia historia inaonyesha kombe la dunia halijawahi kutoka nje ya bara la Marekani ya kusini pindi linapochezwa barani huko.
Kama Uholanzi angetoka historia ya kombe hilo kutobaki Marekani ya kusini ingekuwa imefutika kwa sasa bado ipo mpaka mechi ya mwisho ya fainali Jumapili 13 Julai 2014 nchini Brazil.