WADAU TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HII KAMA ITAKUKWAZA LAKINI NDIO UNYAMA WA BINADAMU WA SASA….KUNA WANAOKESHA USIKU KUCHA WAKIMLILIA MUNGU AWAJALIE KUZAA LAKINI WENGINE WANATUPA WATOTO WASIOKUWA NA HATIA…MO BLOG INALAANI UNYAMA HUU NA MUNGU AWANYIME UZAO KWA WALE WOTE WANAOUA VICHANGA VISIVYO NA HATIA…..Pichani ni Maiti ya kitoto kichanga ikiwa kwenye mfuko wa rambo.
Wakazi wa eneo la Magomeni zilipovunjwa nyumba za KOTA jijini Dar es salaam leo wakishuhudia mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa umri wa siku moja akiwa ametupwa huku akiwa amekufa katika eneo hilo na mtu asiyefaamika. (Picha na Philemon Solomon wa Fullshangwe).
Gari la askari polisi wa kituo cha Magomeni usalama wakiwa katika eneo ambalo ametupwa mtoto mchanga akiwa amekufa kwa ajili ya kuchukua mwili wake na kumpeleka sehemu husika.