
kweli kila jambo lina wakati na muda wake, hivi unahabari kwamba beats ya wimbo wa Yahaya wa Msanii Lady Jay Dee Ulikua utumike katika wimbo mwingine wa Lady Jay Dee aliowahi kuufanya na msanii Mkubwa sana hapa barani Afrika?
Ikiwa Exclusive jana Man water ambaye ndio Producer wa ngoma hiyo alizungumza kupitia mahojoano yake na kipindi cha SonDowner Kinachorushwa na Magic FM akiwa na mtangazaji Mussa Kipanya
Pamoja Na mambo mengine pia lakini man water alitoa siri hiyo ambayo Hata Msanii mwenyewe Wa Wimbo Huo Lady Jay Dee hajawahi kumuambia wala kustukia
Man Water Alisema Beats Ya Wimbo Huo Wa Yahaya Aliitngeneza baada ya msanii Lady Jay Dee Kumpigia simu kuwa angetaka beat yenye mahadhi ya kiafrika kwasababu anataka aitumie katika colabo na Mwanamuziki wa Nchini Zimbabwe Oliva Mtukuzi ikiwa ni miaka kitatu iliyopita
“Unajua ile ngoma, jide alinivutia waya hapa tunaunguza miaka kadhaa nyuma, akaniambia bwana water hebu ni sampie beats yenye mahadhi ya kiafrika afrika maana nataka kufanya kulabo na msanii mmoja mkubwa hapa Afrika, Basi mimi nikaanza kazi mara akanipigia tena ikabidi tu aniweke wazi kwamba msanii mwenyewe ni Oliver Ngomaa, Dah hapo kichwa kikaanza kunizunguka maana niliposikia jina la huyo msanii nikaanza kumfikiria jinsi alivyo mkali na anavyoweza zaidi na yeye ni muandaaji wa muziki ikabidi nitulize kichwa ndio nika sample beats hii inayotumika kwenye wimbo wa Yahaya sasa hivi, sasa ikabidi jide aje aiskilize kabla hajaja kuingiza sauti na Oliver, alikuja na Gadner baada ya kuskiliza daah wakaitolea nje na kusema bado sio yenyewe dah nikawa sina jinsi nikaunda beats lingine likakubalika ndio ukatoka ule wimbo wa MIMI NI MIMI aliofanya Lay Jay Dee ft Oliver Mtukuzi”
Man Water aliendelea kusema “sasa baada ya miaka kadhaa kupita si ndio Jide akaja sasa anataka kufanya ngoma ya yahaya akaniambia e bwana nanna ngoma hapa hebu nipe beats, aaah mi nkasema siwezi buni m beats ukapote hivi hivi nkachukua ile ile aliyoikataa ya kwanza kwenye wimbo wa Oliver na yeye Nikamskliizisha, sasa yeye hapo alishaisahau kwasababu ni muda kidogo ulipita, mi nikakomaa nayo hii ndio kali basi akiwa studio mi naipiga piga ili aizoee maskion mara akavutiwa nayo akaikubali na ndioo hii imekuwa hit katika wimbo wa Yahaya ambao nao ni moja ya list ya ngoma za jide zilizopo kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za kili mwaka huu” alimalizia kusema
Water Aliwakumbusha kwa kuwaomba washabiki wake na wa muziki mzuri na watanzania Nzima kuweza kumpigia kura kama mtayarishaji bora wa muziki kw mwaka 2014 kinyag’anyiro kilichomuweka juu baada ya nyimbo kama Joto Hasira Wa lady Jay Dee, Yahaya, Tupogo ya Ommy akiwa ameshiriki ka asilimia nyingi kuutengeneza na nyinginezo kufanya vizuri kwa mwaka husika huku nazo zikitajwa kuwania tuzo katika vipengele tofauto tofauti
Mpigie Kura man Water kwa kuandika kupitia sehemu yako ya messege BK2 kisha tuma kwenda 15440
