
Pamoja na Sababu alizozitaja katika waraka wake aliouandika na kuutoa kupitia ukarasa wake wa Instagram kuwa “NIMEAMUA KUBADILISHA JINA LANGU KUTOKA ‘DIVA BOSS LADY’ KUWA’ OFFICIAL JACKIE CLIFF’ NA HII NI KUTOKANA NA WIMBI LA MABOSS LADY WALIYOIBUKA NA KUTUMIA JINA HILO NDANI YA MTANDAO HUU A INSTA, SASA KUWA HURU KUTUMIA JINA HILO TANGU SAA SITA KAMILI YA 24 JULY, MIMI RASMI NI OFFICIAL JACKIE CLIFF”
Hivyo ndivyo unavyoweza kutafsiri namna alivyoandika waraka huo kutoka katika lugha ya kiingereza aliyoitumia.
baada ya kuona hivyo website hii haikuridhika ikabidi imtafute Jack mwenyewe ili aweze kuelezea kwa kirefu zaidi kuhusiana na maamuzi hayo magumu aliyoyafanya ikiwa tayari jina hilo lilishazoeleka sana kwakwe.
Nilipata fursa ya kuzungumza na Official Jackie Cliff kuhusiana na maamuzi yake hayo siku ya Iftar ya Women Suport Women pale Msasani Mall bila kusita baada ya kumuuliza Aslisema kuwa jina hilo alipewa na mume wake walioachana hivyo haoni sababu ya kuendelea kulitumia, hata hivyo maisha yake ni yale yale nyumba anayoishi ni ilele ile Gari anayoendesha ni ileile so sio kwamba amefulia ndio maana akaamua kujitoa katika Uboss.
Pia alimtaja Mtangazaji mmoja maarufu liyezidisha kumtia kichefuchefu baada ya kuanza kujiita jina hilo bila haya huku akijua Diva Boss Lady ni mmoja tu Tanzania.
hata hivo baada ya kumuuliza sababu za kuachana na mume wake alisema kuwa aliamu tu bila kutoa maelezo ya ziada.
hivyo Basi kuanzia usiku wa tarehe 24/07/2013 ambayo kwangu nasherehekea kama siku ya kuzaliwa mtambue aliyekuwa Diva Boss Lady kama OFFICIAL JACKIE CLIFF.
Habari ndio hiyo.
