Wakati kamati za bunge maalumu la katiba zikitarajia kuwasilisha ripoti zao bungeni mjini Dodoma huenda zoezi la wabunge kipigia kura vipengele vya sheria likasisimama kutokana na muda endapo rais hataongeza muda wa majadiliano wa bunge hilo.
Mwenyekiti wa bunge malaamu la katiba Mh. Samweli Sita amesema hayo jijini Dar Es salaam katika ziara yake ya kukutana na viongozi wakuu wa dini nchini kwa lengo la kuwapa taarifa juu ya mchakato mzima wa bunge hilo amabpo amebaini kuwa ni vipengele viwili pekee vinavyohusu muungano ndivyo vilivyojadiliwa kati ya vipengele kumi na saba na kuwa tarari ameshakutana na rais Kikwete kumwomba aongeze muda wa bunge hilo jambo lililoonesha kukubaliwa na Rais.
Aidha mh sitta ameongeza kuwa kamati kumi na mbili zilizoundwa zinatarajia kuwasilisha ripoti zake alhamis tarehe 10 mwaka huu na baadae wabunge wa bunge hilo watapata fursa ya kuzijadili huku ukomo wa siku 70 zilizotengwa kwa majadiliano ya bunge hilo zikitarajiwa kufikia ukomo tarehe 28 aprili na huenda shughuli hizo zikaahirishwa kwa ajili ya kupisha bunge na baraza la wawakilishi kwa ajili ya bajeti kwa serikali zote mbili bara na Zanziba.
Baadhi ya wasomi nchini licha ya kupongeza zoezi la mchakato mzima wa bunge hilo wamesema swala la muda sio la muhimu sana ukizingatia umuhimu wa upatikanaji wa katiba na kuitaka serikali kutambua kuwa demokrasia ni ghali hivyo lazima gharama itumike ili ipatikane katiba itakayozingitia misingi ya kidemokrasia.