Wafanya biashara ya nyama wagoma baada yakupewa masharti makali ikiwemo kuweka viyoyozi ndani ya mabucha yao mkoani Kilimanjaro…
baada yakufanyiwa ukaguzi katika mabucha hayo sita kati ya 50 yamebainika hayana vigezo kati ya mabucha 50 yaliyopo mkoani Kilimanjaro..,
wakazi wa mkoa huo wamesema kwa siku mbili hawajapata kitoweo hicho.
Akizungumza kwa niaba yawafanyabiashara wenzake Damiani Temba amesema wameamua kufanga mabucha hayo kutokana na manispaa kuwapa masharti magumu ambayo si rahisi kutekelezeka..,
masharti hayo ni pamoja na kuweka viyoyozi,kuweka msemeno maalumu,leseni ya TFDA pamoja na mabucha hayo kuwa na vioo..