Kapteni Hannah Winterbourne amekuwa afisa wa kwanza duniani kubadilishiwa jinsia. Hannah alizaliwa akiwa mwanaume na alitumia miaka yake ya mwanzo jeshini akiwa kama mwanaume kabla ya kuamua kufanyiwa upasuaji wa kubadili
jinsia akiwa nchini Afghanistan mwaka 2013. Kwa sasa Hannah ndiye mwanajeshi aliyebadili jinsia mwenye cheo kikubwa zaidi jeshini na pekee kuwa afisa wa jeshi,Kwasasa Hannah anaongoza kikosi cha
wanajeshi 100. “Nafikiri mwanzo watu wengi walipata mshtuko, wengi hawakutegemea hiki nilichokifanya kwasababu si kitu cha kawaida kutokea katika jeshi. Hatahivyo muda si mrefu watu wataelewa kwamba kubadili kwangu jinsia hakuathiri utendaji wangu wa kijeshi, mwisho wa siku bado ninaweza kuyafanya yale yote niliyokuwa nikiyafanya kabla sijachukua uamuzi huu.” “Jeshi la Uingereza ni mwajiri mzuri kwa watu waliobadilisha jinsia, tangu mwaka 1999 tuna sera nzuri ambazo zipo wazi kabisa” Filamu inayozungumzia maisha ya Hannah imewekwa katika mtandao kama moja ya kampeni ya kuelezea maisha ya watu waliobadili jinsia zao maarufu kama transgender.