Mkali wa ngoma ya Wrecking Ball mwanadada ambaye anafuata nyayo za Riri imesemekana anatoka kisirisiri na producer wake aliyemtengenezea albamu zake zilizofanya vizuri kwa miezi nane sasa, mshikaji anafahamika kama Mike Will Made It, vyanzo vya stories hii vimetokea kupitia Us Weekly.
“Kila mtu aliyekaribu naye anajua wamekuwa pamoja kipindi chote” Kilisema chanzo ambacho ni mtu karibu wa Cyrus mwenye miaka 21.
Mara ya kwanza walionekana kuanza kutoka pamoja na producer huyo mwenye miaka 25 mara tu baada ya kuachana na mpenzi wake Liam Hemsworth Septemba 2013.
Mtu mwingine wa ndani kabisa amesema kwamba wawili hao wamekuwa serious. Producer huyo ambaye ameshatengeneza hit 23 amefanikiwa pia kukubaliwa na mama mkwe Tish Cyrus mama yake na Miley Cyrus, Tish amesema nay eye ni sehemu ya familia hiyo.