Kote duniani zaidi ya wasichana milioni 30 wako katika hatari ya kukeketwa katika kipindi cha miaka kumi ijayo, kulingana na shirika la Unicef.
Utamaduni huo unafanywa na jamii za watu katika Mashariki ya kati,Afrika na Asia na ni tatizo linalokithiri katika mataifa mengi ambako wanahamia.
Moja ya nchi zilizoathirika ni Uingereza ambako serikali inajaribu kukomesha utamaduni huo
Hata Hivyo inaelezwa kuwa sababu hiyo ni kutokana na Ungereza kuwa na jamii nyingi kutoka mataifa mbali mbali inayoishi hapo hivyo imani na tamaduni nyingi zinaamini ukeketaji ni tendo bora kwa msichana anayeandaliwa kuolewa jambo ambalo si sahihi
Mawaziri nchini uingereza wamekuwa mstari wa mbele kabisa katika swala hilo la la kutokomeza ukeketaji huku kukiwa na vituo vya afya vinavyo saidia waathirika wa ukeketaji kwa kupiga simu bure na kupewa ushauri nasaha
Hakuna Kesi hata moja iliyoripotiwa Rasmi japo Takwim Zinajionyesha ni Tatio kubwa sana