Kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela akionyesha moja ya silaha walioyofanikiwa kuikamata katika Operesheni hiyo.
Katika operesheni za kupambana na uhalifu zinazoendelea katika mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Jeshi la polisi likishirikiana na askari mgambo na ulinzi shirikishi kutoka manispaa ya kinondoni limefanikiwa kuwakamata jumla ya wanawake 51 wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya kujiuza kimwili hadharani.
Wanawake hao wamekamatwa katika maeneo ya Msasani Mikoroshini, Mwananyamala, Kinondoni Barabara ya Tunisia, Sinza Corner Bar na maisha Club.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela amesema wanawake hao pia hutumika kuwapora mali wanaume kwa kuwawekea madawa ya kulevya katika vinywaji, vyakula na hata katika miili yao na pia kushirikiana na wahalifu wakiwemo majambazi katika kufanya matukio ya aina mbalimbali ya kihalifu.
Story na Mo blog Team