Meneja huyo akaendelea kusema, ilipofika saa tano usiku, Wema na marafiki zake walionekana kuzidiwa na kilevi, wakaanza kufanya fujo kwa kupiga kelele, kitendo kilichowakera wateja waliokuwa katika mgahawa huo, wengi wakiwa ni Wazungu ambao waliondoka kutokana na fujo hizo.
Aliongeza kuwa mmoja wa marafiki wa Wema ambaye ilidaiwa ni mpenzi wake, aliyejulikana kwa jina moja la D, alichukua glasi na kuipasua chini kwa makusudi huku meneja huyo akishuhudia.
Meneja akasema: Wakati wanaondoka, nilimfuata yule jamaa mpaka nje, nikamuuliza ni kwa nini amevunja glasi kwa makusudi, akanijibu kwa dharau huku akinitukana na kutishia kunipiga, akawa ananiuliza hiyo glasi ni shilingi ngapi kwani ?.
“Niliamua kupiga simu Kituo cha Polisi Kawe, wakaja kuangalia mazingira kisha nikaondoka nao kwenda kufungua kesi kituoni.”
4 Comments
kazi yako una copy na ku paste kwenye blog zingine.
hiyo nayo kazi Aisha kama ulivosema mwenyewe… jaribu uone kama ni rahisi. Alafu usikwazike sana unataka kuona nini hapa nikuwekee cha tofauti na wengine
salma unajitahidi sana,congrats,mana twapata habari zikiwa latest kabisa
pendo chasama Nashukuru sana mpenzi kutembelea na kufurahiya Website yangu. Thank You so much