Mwanamziki mashuhuri wa muziki wa ‘pop’ kutoka Canada Justin Bieber amefunguliwa mashtaka ya kumpiga dereva wa gari la kifahari la kukodisha mwezi Disemba mwaka uliopita.
Bwana Bieber aliye na umri wa miaka 19 alikaribishwa katika katika kituo cha polisi cha Toronto baada ya kujisalimisha mwenyewe ..Amefunguliwa mashtaka chini ya juma moja baada ya kukamatwa mjini Florida marekani kwa shutuma za kuendesha gari akiwa mlevi na mashtaka mengine likiwemo la kufanya mashindano ya magari yasio maalum huku akitumia pia leseni iliyokwisha muda wake
Kwa mujibu wa polisi wa Toronto, yapata saa 02:50 saa za Canada tarehe 30 Dicemba, gari la kifahari liliwasili kumchukuwa Bieber na wenzake watano katika kilabu moja ya starehe ili kuwarejesha katika chumba chao cha hoteli.Na wakati walipokuwa njiani, dereva huyo pamoja na mmoja wa abiria wake, aliyetajwa kwa jina la Bieber, wanasemekana kuanza kufokeana maneno makali.
Abiria huyo “alimgonga dereva wa limousine hiyo kwenye kisogo mara kadhaa”, polisi wamesema….Dereva huyo anasemekana kusimamisha gari lake na kisha kutoka nje na kuwaita polisi. Mshukiwa ‘alichana mbuga’ kabla ya polisi kuwasili.
Bieber kweli kauanza mwaka vizuri pamoja na ngoma yake aliyoitambulisha hivi karibuni ya “CONFIDENT” sio ishu midomoni mwa watu ishu ni kuwa mgeni wa vituo vya police kila kukicha
Ujana maji yamoto, inavyoonekana Bieber anasumbuliwa na FOLISH AGE nahisi anahitaji ashauri shupavu