
Ndege Ya Mwanamuziki Justine Bieber Kwenye Ukaguzi wa police Mwanamziki Justine Bieber aingia matatani tena baada ya polisi kusachi ndege yake binafsi baada ya polisi hao kuwa na wasiwasi huenda atakuwa abeba bangi Ndege hiyo ilianza kusachiwa tu baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa New Jersey.
Polisi waliendesha msako mkali katika ndege hiyo na baada ya kukosa walichokuwa wanatafuta waliruhusu ndege hiyo kuondoka. Mwanamuziki huyo amekua akiandamwa na majanga ya kukamatwa na kushtakiwa kwa makosa mbali mbali tangu mwaka huu uanze
