Katika maisha unapoamua kufanya kitu inatakiwa ukifanye na kama unakipenda basi ndo ukifanye kwa bidii iko siku mambo yatakuwa fresh never give up.
Ni miaka 20 toka mkali Warren G alipotoa albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Regulate, unaweza ukapiga hesabu 20 years back ulikuwa wapi ni siku nyingi aisee. “ilikuwa fresh sana nilikuwa shule ya msingi nikawa navaa koti la Dre naenda nalo shule” alisema Warren G wakati akipiga stories na kipindi cha Dj Skee kinachoitwa SKEE Live akaongelea mafanikio ya mwanzo kabisa ya Dre ambae kwa sasa ni hip hop artist anaeongoza kwa mkwanja.
Warren G pia aliongelea uhusiano wake na Snoopy Doggy utotoni pamoja na kujifunza jinsi ya kunyonga beats kutoka kwa kaka yake Dre. “Sikuwahi kufikiria ingefikia ukubwa huu, nilikuwa nikipenda muziki tu nikawa nataka watu wa kawaida tu kitaani ndo wasikie lakini haikuwa hivyo muziki wangu ulisambaa kila mahali duniani” alisema Warren G.
Akiwa na miaka 18, 17 hivi alimuomba Dre amueonyeshe jinsi ya kutumia MPC 60 na alimuonesha, na baada ya hapo mshikaji akaendelea kufanya kwa sababu alitaka zaidi kujihusisha na mambo yaliyokuwa yakiendelea kwa kipindi kile badala ya kufanya deejaying tu. Ingawa alishawahi kurap na Snoopy siku za nyuma wakiwa na crew inaitwa Voltron.
Warren G na Snoopy wamesoma pamoja, alikuwa Snoopy Warren G na kaka yake anayeitwa Jerry, licha ya kwenda shule moja walikuwa majirani, Snoop aliishi 19th and Lewis na Warren G aliishi 21th and Lewis, walikuwa wakicheza pamoja, baada ya kukua taratibu wakaanza kutengana, lakini siku moja akiwa Jordan High school wakati wa chakula cha mchana akamsikia mtu anamuita kugeuka akakuta ni Snoopy, akamuuliza Snoopy unafanya nini pale? Ndipo walipoungana tena pale tena ndo mpaka leo wanatisha katika gemu.
“Anasema Snoopy aliendelea kukaa na Snoopy sana huku akiendelea kurap, bila kukata tamaa, ingawa walikuwa na hali ya maisha tofauti lakini waliamua kukaa pamoja katika njia sahihi angawa hawakuwa na pesa bado lakini waliendelea kukomaa paka leo hii wametusua.