Kanye West siku ya jana kweli alipanic baada ya kukimbizwa hospitali huko Australia, lakini taarifa za channel ya E zinasema kwamba Kanye anaendelea vizuri kwa sasa.
Alikimbizwa hospitali lakini hakuwa na serious health problem ila ni kitu kinachofahamika kama migraine, ni maumivu ya kichwa ambayo muda mwingine hupelekea kutapika na hutoa dalili kuwa mwili haupo sawa, husababisha uhisi vibaya na alipelekwa hospitali kama precaution.
Taarifa zinaeleza mume huyo wa Kim Kardashian aliendelea kufanya tour yake ya Yeezus masaa machache baada ya kutoka hospitali.
Taarifa za E! News zianeleza kwamba Kanye baada ya kupata huduma akiwa hospitali, kwa sasa anaenjoy kwenye hotel huko Sydney akiwa na mke wake Kim na mtoto wao North West.
Kanye anashow 2 zilizopangwa kufanyika Sydney baadae wiki hii.
Kanye West hakutweet kuhusu kukimbizwa hospitali, lakini Kim alipost picha akiwa na West usiku mmoja huko Melbourne.