
Kendrick Lamar ambae ameripotiwa kufanya kazi kwa ajili ya albamu yake inayokuja baada ya albamu ya good kid, m.A.A.d city, juzi kati alifunguka akasema kuna ngoma ambazo hazikuachiwa kutoka kwenye albamu hiyo wakati wa kurekodi.
“”Kulikuwa na ngoma kibao zilizoachwa, ingeweza kuwa albamu ya ngoma 30, kuna ngoma chache ambazo zinaweza zikaendana na nilichokuwa nikiongelea” alisema Kendrick wakati akipiga stories na Rolling Stone taarifa za Rap-Up zimeeleza.
Kendrick Lamar anasema kuna ngoma ambazo anazifanya na Dr. Dre kwa ajili ya albamu yake mpya, pia aliongeza kwamba Dr. Dre ameingia studio na alijaribu kujiongeza, Lamar kufanya kazi na Dre ni jitihada za K.Dot mwenyewe na watayarishaji wengine wa mapigo ya muziki.
Lamar ambae alikuwa na Drake kwenye albamu ya good kid anasema hatakuwa na featuring kwenye albamu yake inayokuja. “ Ninayo mengi sana ya kusema, hiyo ndio uchoyo wangu mkubwa” alisema Kendrick Lamar.
Lamar amesema albamu yake maudhui yake yatakuwa ni hasira na hisia, bado hajataja siku ya kutoka albamu hiyo.
