Akifunguka Mathew Knowles baba yake Beyonce amesema mapigano kwenye lifti ya hoteli kati ya Solange na Jay Z mwezi Mei ilikuwa ni trick ambayo ilisababishwa ili kuzidisha mauzo ya tiketi na albamu.
Mathew pia amefunguka kuhusu kuungana tena Destiny Child kwa ajili ya tour ya Destiny Child ambayo inafanyiwa kazi kwa sasa.
“Mauzo ya tiketi yaliongezeka na albamu ya Solange imeuza hadi asilimia 100” amesema Mathew Knowles wakati akipiga stories na 104.1 KRBE.
Kufuatia kutoka kwa video ya mapigano yale, Solange aliona mchezo katika kuongeza mauzo ya albamu yake kidigitali.
Kutokana na Nielsen Soundscan data zilizopatikana na Hip Hop Dx mwezi Mei albamu yake ilikuwa imeuza copies 600 wiki moja kabla wajapigana kwenye lifti na baada ya mapigano yale mauzo yaliongezeka hadi copies 2,000 katika wiki ambapo walipigana kwenye lifti.
Katika kuongezea kwenye kuongelea ugomvi ule kati ya Jay Z na Solange pia ikatoa dalili za kuungana tena kwa Destiny Child na kufanya concert na albam ambayo yupo Beyonce, Kelly Rowland na Michelle Williams.
“Bado ni meneja wa Destiny Child na ukiona Destiny Child kwenye TV na unawaona wanafanya ngoma pamoja taratibu taratibu, na sasa wameshafanya, siku za karibuni walikuwa kwenye TV station, sijui, inaweza ikawa albamu nyingine ya Destiny Child inakuja, pia inaweza kuwa tour ambayo inaweka historia, ambayo inawashirikisha memba wa Destiny Child akiwemo Beyonce, Kelly na Michelle, unaweza kufikiria jinsi itakavyokuwa? “ alisema Mathew Knowles.
Ukitaka ujue ilikuwa ni deal ambapo familia wamekaa na wanajua wanchokifanya Beyonce aliachia ngoma juzi kati akiongelea mapigano yale ngoma inaitwa Flawless ikiwa ni remix amemshirikisha Nicki Minaji, Beyonce anarap “Up in this shit like elevators. Of course some shit go down when there’s a billion dollars on an elevator.”
Mpaka hapo inaweza ikawa bado ni deal lakini yote kwa yote ukweli wanaujua wao, kama kulikuwa kuna la zaidi ya hilo kama sio deal iko siku tutajua.