Wakati juhudi za kuisaka ndege iliyopotea ilipokuwa ikisafiri kutoka Malaysia kuelekea Uchina zikiendelea, ndege moja ya Vietnam imeripoti kuwa imeona kitu kinachofanana na mlango wa ndege kwenye ufuo wa bahari ya Kusini mwa Uchina kwenye mwambao wa taifa hilo.,,Hata hivyo hakuna thibitisho kuwa mlango huo ni wa ndege iliyopotea ya Malaysia, iliyokuwa na abiria mia mbili na thelathini na tisa.
Uchunguzi kuhusiana na kilichosababisha kupotea kwa ndege hiyo mapema siku ya Jumamosi, inawalenga abiria wawili wanaodaiwa kuwemo ndani ya ndege hiyo, waliotumia paspoti iliyoibiwa..
Stakabadhi hizo mbili za kusafiria kutoka Italia na nyingine Australia inaaminika kuibwa nchini Thailand.
Idara ya polisi ya Kimataifa, Interpol, inasema kuwa ni mapema mno kuhusisha pasi zilizoibwa na kutoweka kwa ndege hiyo…,Na huku kushughuli za kuisaka ndege hiyo zikiendelea, Msemaji wa shirika la ndege la Malysia amewaambia jamaa ya watu waliokuwemo katika ndege hiyo, kujiandaa kwa taarifa mbaya.