Mamlaka ya wawasiliano Tanzania TCRA kupitia kamati ya maudhui imevifungia vituo viwili vya radio na kukipa onyo kituo kimoja cha radio pamoja na kulipa faini ya shilingi milioni tano baada ya kukutikana na makosa kadhaa ya ukiukwaji wa maadili katika utangazaji.
Akizunguza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti kamati ya maudhui ya TCRA Bw. Walter Bgoya ambaye alikuwa ameambatana na wanakamati wa kamati ya maudhui kutoka TRCA, amevitaja vituo vya radio vilivyofungiwa ni Radio Iman Fm inayoelezwa kuwa ilitoa matamshi ya kiuchochezi ya kuhamasisha waislam kutoshiriki zoezi la sensa lilifanyika mwaka jana, ambapo Radio ya Kwa Neema Fm imefungiwa kwa kosa la kutoa matamshi ya kiuchochezi dhidi ya mgogoro wa kuchinja nyama ulioibuka hivi karibuni kati ya waislam na wakristo.
Bw Bgoya ameeleza kuwa baada ya kukaa vikao na uongozi wa kamati ya maudhui wa TCRA pamoja na baadhi ya viongozi wa radio hizo na kujiridhisha kuwa kulikuwepo na ukiukwaji wa kimaadili kwa baadhi ya watangazaji wa vipindi vilivyotajwa ambapo inadaiwa walitoa matamshi ambayo yanaelezwa kuwa ni yakiuchochezi kwa jamii na kuonekana kuwa ni kinyume cha kanuni na sheria za utangazaji za
mwaka 2005.
Aidha Radio Clouds Fm nayo imepewa onyo kali na kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni tano ndani ya mwezi mmoja pamoja na kufuta kipengele cha Jicho la ng’ombe katika kipindi cha Power breakfast ambacho kinaelezwa kuwa kilikuka maadili ya utangazaji kwa kutoa matamshi ya kiuchochezi yanayozungumzia ushoga mnamo tarehe 23/01/2013 wakati wa kuapishwa kwa Rais wa marekeni Barack Obama.
Kwa mujibu wa Mamalaka hiyo kupitia kamati yake ya maudhui imeeleza kuwa viongozi wote wa radio zilizoripotiwa kuhusika na makosa hayo ya kiutangazaji waliandikiwa barua na kutakiwa kujieleza mbele ya viongozi wa kamati ya madhui TCRA , na baadaye kukiri kuwa kulikuwa na baadhi ya makosa ya kiutangazaji katika kufikisha ujumbe kwa jamii na hivyo kukiuka kanuni za utangazaji na maadili ambazo zinamtaka kila mwenye leseni ya utangazaji ajiepushe na mambo ya Udini, Ukabila, Rangi, na Utaifa bali azingatie katika mambo yafuatayo ikiwemo maslahi ya taifa, umoja wa kitaifa, na uchumi wa taifa.
Mbali na adhabu zote zilizotolewa na kamati hiyo pia imevitaka vituo hivyo kukiri kwa barua kutofanya tena makosa hayo na kutakiwa kuwaonya watangazaji wao kujiepusha na matamshi ya kiuchochezi na endapo vitakiuka tena basi kamati hiyo haitasita kuivifungia kabisa vituo hivyo kwa maslahi ya taifa na kwamba Rufaa iko wazi ndani ya siku thelathini.
Story by Upendo Msuya.