Ludacriss amepangwa kupewa heshima kwa ajili ya kazi inayofanyawa na Ludacriss Foundation, Ludacris atapewa tuzo hiyo ya rais kutoka kwa BMI.
“Tuzo ya BMI ya rais ni zawadi kubwa kwa watu ambao wamefanya vitu na kufanikiwa katika jamii pia kwa kuandika nyimbo zikiwa na mafundisho juu ya tamaduni ya mahali husika na katika ulimwengu wa burudani kwa wakati mmoja bila kupoteza maana na katika kusaidia jamii kwa ujumla” Alisema Mike O’Neill rais na C.E.O wa BMI ambao watampa Ludacris heshima hiyo.
Nae makamu wa rais wa BMI Catherine Brewton alirudia katika kumsifu Ludacris na kusema ni shujaa wa mji wa nyumbani mpaka kwenye jiji la Atlanta, amekuwa na mafanikio makubwa katika muziki, filamu na televisheni, yuko imara katika kazi yake na pia katika kusaidia jamii kwa ujumla, hii inadhihirisha ni zaidi hata ya kupokea tuzo ya rais kutoka BMI.
Ludacris ana albamu nyingi ikiwemo ya mwaka 2000 ya Back for the first time, Word of Mouf ya mwaka 2001, Chicken and Beer ya mwaka 2003, Red Light District ya mwaka 2004, Release Therapy ya mwaka 2006, Theater of The Mind ya mwaka 2008, na Battle of the sexes ya mwaka 2010 na kwa sasa Luda anatengeneza albamu ya Ludaversal.
Tumeshasikia mambo kibao ya kijamii ambayo yanafanywa na Ludacris Foundation ni jambo zuri hata wasanii wengine nao wanafanya lakini Ludacris ameonekana yeye anakwenda mbali zaidi na hata kupewa President Award ikiwa ni kichocheo kwa wasanii wengine nao kujitoa na kuweza kusaidia jamii hata kwa aina ya mashairi yao wanayoandika yakiwa yanatoa moyo kwa wale wasio na mahitaji muhimu hapa duniani….Congrats Luda.
Ludacris Kushinda Tuzo Ya BMI Ya Rais
Related Posts
-
-
Albamu 20 Bora Za Hip Hop Ndani Ya Miaka 20 Hizi Hapa
-
How Sweet, Flaviana Matata Is Official Taken “Achumbiwa”
-
Pole Kwa Msiba Wa baba Mzazi, Maddam Wema Sepetu
-
20% IS BACK NA MALI ZA URITHI
-
Peter Wa P.Square Asherekea siku Yake Ya Kuzaliwa
-
Tazama Video Jinsi Hemed PHD Alivyonusurika Kutandikwa makofi jukwaani na Mrembo Aliyemtomasa na Kumpulizia Spray Kinyemela