
Mangwea akiwa na M to the P
Taarifa zilizothibitishwa kutoka nchini Afrika Kusini ni kwamba yule msanii aliyepelekwa hospitali pamoja na Mwana Hip Hop, Albert Mangwair aitwaye M to the P naye amefariki dunia leo.
M2 the P alipelekwa katika hospitali ya St Hellen iliyopo jijini nchini humo kwa matibabu baada ya kukutwa amepoteza fahamu akiwa na Mangwair aliyefariki dunia jana.
Miili ya marehemu hao bado ipo katika hospitali ya St. Hellen na mipango ya kuhamisha miili hiyo bado inaendelea hivi sasa.
Taarifa zisizo rasmi zinadai kuwa yawezekana Mangwair na M2 the P walikula chakula chenye sumu ambacho kimepelekea mauti hayo.
Baadhi ya Watanzania waishio nchini Afrika Kusini wamejikusanya kwa ajili ya kuandaa mipango ya kuhifadhi miili hiyo pamoja na safari ya kuileta nchini Tanzania.

1 Comment
we nae na habari za uongo umesomea shule gani wewe jamani kumuua mtoto wa watu inahusu nini another fake information