
Ilikuwa ni tukio kubwa baya ambalo liligusa dunia, lilitokea miaka 50 iliyopita baada ya ndege hiyo kupotea baada ya kupata ajali huko Chile ikiwa imebeba wachezaji na haikujulikana ilienda wapi.
Taarifa za Mailonline zinasema kwamba wapanda mlima katika mlima wa Andes walikuta mabaki ya ndege hiyo ambayo ilianguka Aprili 3 mwaka 1961 ikiwa na watu 24 ndani yake.
Ndege hiyo mabaki yake yamepatikana na wapanda mlima hao wamekuta mabaki hayo ikiwa ni mita 190 kusini mji mkuu wa Santiago.mifupa ya watu ilikutwa kukiwa na mabaki ya ndege hiyo pia.
Katika picha zilizopigwa zinaonyesha eneo la ajali hhiyo ikionyesha vipande vipande vya ndege hiyo vilivyokaa kwa miaka 54 katika mlima huo. Timu hiyo ilikuwa imeshacheza mechi ya nje huko Osorno katika kombe la Copa de Chile na ilikuw aikirudi kuelekea Santiago baada ya kutoka droo 1 – 1.
Ndege hiyo ilikutwa mita zaidi ya 3,2000 juu ya kwenye mlima huo.
