
Wale wasichana wawili wa kihindi waliokutwa wamening’inia mtini mwezi may hawakuw wmeuliwa bali walijiua wenyewe ikiwa ni ripoti ya upelelezi toka kituo cha Bureau
Wapwa hao Pushpa mwenye umri wa miaka 15 na Murti mwenye miaka 14 walipotea mwezi may 27 baada ya kuwaaga wazazi wao kuwa wnakwenda kutumia vyoo vya jirani kujisaidia
Baadae Mabinti hao walikutwa wamening’inia katika mti wa muembe katika kijiji cha Uttar Pradesh
Iliaminika mabinti hao walibakwa na hatimae kunyongwa mpaka kufariki na genge la wahuni vijana watano wa kihindi jamnbo ambalo limeonekana si la kweli CBI imesema
‘Ndio, Tumefanya uchunguzi na imeonekana Mabinti hao walijiua na hawakuuwawa'” Mkuregenzi wa CBI Ranjit Sinha amesema t
Taarifa Hiyo ya CBI Imeongeza kuwa Mabinti hao hawakufanyiwa vitendo vyovyote vya ubakaji Kwa mujibu wa vipimo vya vinasaba DNA test na uchunguzi wa kidaktari uliofanywa kwenye miili hiyo.
