Madereva wa malori zaidi ya mia tatu wamegoma kuendelea na safari katika barabara kuu itokayo Dodoma hadi Mwanza baada ya dereva mwezao aliyekuwa akiendesha lori kuvamiwa na majambazi katika eneo la kisaki manispaa ya Singida.
madereva ambao wamekutwa katika eneo hilo wameomba jeshi la polisi kufanya doria mara kwa mara eneo hilo kwani kumekuwa na matuki yanayo jirudia ya utekeji wa magari kwa kuweka mawe makubwa barabarani na kuwajeruhi madereva jambo ambalo lina tishia amani kwa watumiaji wa barabara.
Madereva wa malori baada ya kufunga barabara naibu waziri wa Afrika mashariki Dr. Abdulla Abdulla alikumbwa na adha hiyo na kusema ni haki ya kikatiba kwa madereva kugoma kwa kudai haki zao, kutokana na hali hiyo amewahaidi madereva kupeleka kilio chao katika mamlaka husika ili kuweza kutatua tatizo lao na kukomesha vitendo vya uvamizi wa magari katika eneo hilo .